Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Bwana Ahmad Zahid Hamidi, katika hotuba aliyotoa kwenye sherehe za ufunguzi wa mkutano maalumu wa Qur’ani Tukufu, alisisitiza kwamba: mikakati yote na mifumo ya kuweka sheria za kijamii, kiutamaduni na kiuchumi katika jamii lazima iathiriwe na Qur’ani.
Akaongeza kuwa: “Hivi leo tunaishi katika dunia yenye kasi kubwa mno ya maendeleo ya teknolojia na ubunifu mpya, na tunaona majengo marefu (maghorofa) yakiongezeka urefu kila uchao, na ukuaji wa kiuchumi na kielimu ukisonga mbele kwa kasi, tukio hili limepelekea roho ya binadamu kuwa na wasiwasi mkubwa, matokeo yake, maadili yamedhoofika kwa kiwango fulani, na uelewa wetu wa ubinadamu umepungua, katika hali hii, kinachokuja kuokoa roho ya mwanadamu si kingine ila ni kitabu hiki cha mwongozo wa ubinadamu, Qur’ani!”
Naibu Rais wa Malaysia alibainisha kwamba: “Mkutano huu maalumu si jambo la kikao cha kugawana mawazo pekee, bali kwa hakika ni wa kusonga mbele katika mijadala ya Kiislamu, kwahiyo tusiruhusu matokeo yake yabaki kwenye kurasa za karatasi na kumalizika hapo; bali lazima tuyatekeleze matokeo yake kivitendo katika jamii.”
Mkutano huu maalumu ulikuwa na washiriki 1,500 wa kielimu na wenye umahiri wa hali ya juu, waliokusanyika kwa lengo la kuimarisha nafasi ya Qur’ani katika maisha ya kila siku.
Chanzo: Bernama
Maoni yako